Entertainment

Lady JD Afungukia Tetesi Za Kuachana na Mpenzi Wake

Promote/Advertise with us!! Call/Whatsapp: +234814 964 3802

JAY-dee.jpg

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva mrembo Judith Wambura maarufu kama Lady Jay Dee amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye na mpenzi wake msanii kutoka nchini Nigeria Spicy hawajaachana.

Tetesi za wawili hao kuachana ziliznza baada ya kutoonekana pamoja kwa muda mrefu lakini pia hata mitandao ya kijamii hawakuonekana wakiposti mapicha picha ya mahaba kama ilivyokuwa siku za nyuma.

Kwenye mahojiano na kituo cha habari cha East Africa, Lady Jaydee amesema kwamba hajaachana na Spice, isipokuwa wawili hao wanafanya kazi ambayo inawalazimu kuwa mbali mbali kwa muda mrefu, ikichangiwa na kuwa raia wa nchi mbili tofauti.

Unajua sisi ni wanamuziki, na wanamuziki ni watu wa kusafiri, na hatuishi nchi moja, kwa hiyo yeye yuko kwenye kazi zake na mimi nipo kwenye kazi zangu, ni sawa na mume na mke, mume anaenda kazini na mke anaenda kazini kwake, haimaanishi kila siku muwe mnafuatana, leo hayuko hapa lakini ni mtu ambaye nashirikiana naye kwenye mambo mengi, kama kunisaidia kumpata UTI na kuhakikisha amefika hapa Tanzania”.

Lakini pia Jaydee ameendelea kwa kusema kwamba licha ya Spicy kuwa mbali, amechangia kwa kiasi kikubwa kuweza kufanikisha tamasha la #VocalsNight2018, kwa kuweza kumuunganisha na msanii UTI ambaye  alikuwa MC wa siku ile.

Promote/Advertise with us!! Call/Whatsapp: +234814 964 3802
Click to comment

Leave a Reply

To Top